top of page

Mshukiwa, Dylann Roof akamatwa

Writer's picture: Orina OntiriOrina Ontiri

Mshukiwa wa mauaji ya watu tisa katika Kanisa lenye waumini wengi kutoka jamii ya watu weusi la Charleston, nchini Marekani, aliyetambuliwa kama Dylann Roof, kijana mzungu mwenye umri wa miaka 21,ametiwa mbaroni.

Mshukiwa, Dylann Roof, ni mkazi wa jimbo la Columbia, mji mkuu wa South Carolina, kusini mashariki mwa Marekani, kwa mijibu wa FBI, iliyonukuliwa na Gazeti la kila wiki la Post and Courier. Columbia iko kwenye umbali wa masaa mawili na mji wa Charleston kwa kutumia gari. Dylann Roof alitoweka baada ya kutekeleza kitendo hiki kiovu.

Jambo hili liliweza kuangaziwa alhamisi ambapo  serikali ilipata udadisi kutoka kwa Debbie Dills, ambaye inasemekana alimuona Roof wakati alikuwa njiani kuelekea kazini. Mama huyu alimfuata maili 35 kulingana na the Shelby Star  “nimekuwa nikiwaombea waathiriwa njiani nikielekea kazini” Dills akaendelea kusema. ” nilikuwa mahali halisi katika wakati uliofaa.”

• Akionekana mbele ya koti leo, Roof alishikiliwa hapo Shelby, North Carolina.

Charleston County Coroner Rae Wootenameitambua miili tisa kama ifuatavyo: Cynthia Hurd, 54; Susie Jackson, 87; Ethel Lance, 70; Rev. DePayne Middleton-Doctor, 49; Hon. Rev. Clementa Pinckney, 41; Tywanza Sanders, 26; Rev. Daniel Simmons Sr., 74; Rev. Sharonda Singleton, 45; Myra Thompson, 59.

• yasemekana mhusika alisikika akisema , ” mnachukua wake zetu na kuichukua nchi yetu, mtaenda,” akiripoti Sylvia Johnson, binamu wa mchingaji aliyeuagwa.

Mauaji hayo yalitokea Jumatano saa tatu usiku (saa za Marekani) katika Kanisa la Emanuel African Methodist Episcopal Church, la mjini Charleston, kusini mashariki mwa Marekani. ” Tumeona watu wanane ambao waliuawa ndani ya kanisa “, amesema mkuu wa polisi wakati wa mkutano na vyombo vya habari, kabla ya kubaini kuwa mtu mwengine miongoni mwa wawili waliyojeruhiwa alifariki walipokua wakisafirishwa katika hospiatli iliyo karibu.

0 views0 comments

Recent Posts

See All

Comments


bottom of page