Ni wakati wa kupokea habari za yard na AGR fm lakini kwanza tupate mkhutasari wake
–Naomba wasomi kutembelea shule za kisii kuwaeleza wanafunzi umuhimu wa masomo mbunge Elijah moindi akariri
–Ni maisha na haki yetu kutengenezewa daraja wakaazi wa Gesima waambia serikali ya Nyamira.
1 Mbunge wa eneo bunge la Nyaribari Masaba Kaunti ya Kisii Elijah Moindi amewaomba wasomi wote kutembelea shule zilizoko kaunti hiyo kuwaelezea wanafunzi umuhimu wa mosomo kama njia moja ya kuwatia motisha wanafunzi katika masomo.
Akizungumza siku ya Jumapili katika eneo bunge lake wakati alikuwa akitembelea miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo imetekelezwa kupitia pesa za hazina ya ustawi maeneo bunge CDF Mbunge huyo aliomba wasomi kutembea katika shule za msingi na za upili kuwaeleza wanafunzi maana ya masomo na kuwaelimisha wanafunzi kutia bidii wakiwa katika shule ili eneo la Kisii linawiri zaidi kwa masomo.
Mwakilishi huyo pia aliwaomba wakaazi wa eneo bunge lake kushirikiana na ofisi ya hazina ya CDF ili maendeleo yafanyike zaidi kwa kueleza nini wanakihitaji wafanyiwe katika bunge hilo
2 Wakaazi wa wadi ya Gesima kaunti ya Nyamira wameofya maisha yao kutokana na kuaribika kwa daraja lililoko katika barabara ya kutoka Nyamokono kuelekea Riakworo na maji kupita juu ya daraja hilo na watu kushindwa kupita.
Wakiongea na wanahabari hii leo asubuhi katika eneo hilo la Nyamokono ambapo daraja hilo liko wakaazi hao wakiongozwa na aliyekuwa diwani wa eneo la Gesima Julius Nyachio walisema wameofya maisha yao kwa kushindwa kupita katika daraja hilo ambalo maji yanapita juu na kuomba serikali ya kaunti ya Nyamira kutengeneza daraja hilo kabla maisha ya watu kupotea .
Daraja hilo ambalo hutumiwa na watu wengi zaidi limewazuia wakaazi wa eneo hilo kupita mpaka wanatumia njia ingine badala ambayo iko refu zaidi na wengine ambao ni wafanyikazi hujerewa kufika kwa kazi zao na haswa walimu pamoja na watoto wa shule.
3 Maafisa wa Trafiki pamoja na Askari wa Kaunti ya Kisii wametwikwa lawama kufuatia hali isiyokuwa ya kawaida iliyoshuhudiwa katika barabara zote za kuingilia na za kutoka katika mji wa Kisii.
Wakiongea na kituo hiki baadhi ya wakaazi na wahudumu wa matatu ambao walikuwa wamekwama kwenye msongamano wa magari kwa zaidi ya saa mbili, waliwashtumu Maafisa hao kwa uzembe wanaposhughulikia masuala yanayomlenga mwananchi.
Charles Maina, dereva wa kampuni ya magari ya Mbukinya Travellers aligadhabishwa na utepetevu ulionyeshwa na Askari wa Kaunti hiyo akisema kuwa walikosa kuonyesha uwajibikaji wa kikazi na kuitaka Wizara ya Mipango na Uratibishaji wa mji kuwafundisha jinsi ya kuelekeza magari ili kupunguza msongamano wa magari ambayo imekuwa kero sana kwa wakaazi wa eneo hilo.
Kwa upande wake Jonhstone Mokua ambaye ni mwenyekiti wa Ziwani Matatu Sacco alionyesha kutoridhika kwake kuhusiana na msongamano huo ulioshuhudiwa siku ya Alhamisi ambapo aliwalaumu Mafisaa hao na kudai kuwa walikuwa wanapendea baadhi ya magari ya binafsi hasa wafanyakazi wa kaunti ambao walikuwa wanaruhusiwa kutumia njia mbadala ya RAM hospital ambayo ilichangia msongamano zaidi.
4Bunge la Kaunti ya Nyamira imetenga Sh10 milioni kwa ununuzi wa mitambo ya kurekodi maneno yanayojadiliwa katika bunge hilo, meza za kisasa na viti vya bunge hilo.
Pesa hizo zilitengwa hapo mbeleni kwa ujenzi wa nyumba ya kifahari ya Spika wa Kaunti hiyo pamoja na mkahawa wa bunge hilo, lakini zikabadilishwa kununua bidhaa hivyo muhimu katika bunge hilo kufuatia mswada uliopelekwa bungeni na Mwakilishi wa walio wengi katika bunge hilo Raban Masira na ukapitishwa.
Spika wa bunge hilo Joash Nyamoko aliuunga mkono uamuzi huo na kukubali pesa hizo kutumika kwa kununua mitambo ya kurekodi yale yanayojadiliwa katika bunge hilo.
Wawakilishi wengi waliounga mkono mswada huo na kusema yale wanahitaji katika kaunti ya Nyamira ni maendeleo bali sio kusafiri kama malkia au kuwa na makao ya kifahari.
Sasa ni rasmi kuwa pesa hizo zitatumika kununua mitamnbo katika bunge hilo ambayo itakuwa na manufaa zaidi kwa Wawakilishi hata kwa wakaazi wa kaunti hiyo kuyajua yale hua yanajadiliwa katika bunge hilo kama kumbusho kwa siku za usoni.
Na katika Michezo Kaunti ya Kisii iliebuka na ushindi katika mashindano ya riadha kwenye ubingwa wa shule za msingi ambayo yalianza siku ya Jumapili na kukamilika hapo jana Jumatatu.
Mashindano hayo ambayo yaliandaliwa kwenye uga wa chuo cha Kisii, yalijumuisha kaunti sita kutoka mkoa wa Nyanza, yaliweza kushuhudia kuteuliwa timu ambayo itawakilisha eneo la Ziwa Kuu (Lake Region) katika mashindano ya Kitaifa ya riadha ya shule za msingi ambayo yatafanyika katika uga wa michezo wa Gusii Green.
Akiongea na Yard radio pamoja na AGR, mkurugenzi wa elimu katika kaunti ya Kisii ambaye alikuwa mmoja wa maafisa waandalizi wa michezo hiyo, Bwa Richard Chepkawai alisema kuwa wanalenga kuimarisha michezo yote ya riadha katika kaunti ya Kisii na kudokeza kuwa watahakikisha kuwa wanaboresha matokeo yao zaidi ya jinsi wafanya leo.
Mashindano hayo yalijumuisha shule kutoka kaunti za maeneo Nyanza zikiwemo Migori, Homabay, Siaya, Kisumu, Nyamira pamoja na Kisii, ambao walikuwa wenyeji wa mashindano hayo ambapo vitengo mbali mbali vilishindaniwa kama vile mita elfu 10, mita 400 kupokezana vijiti miongoni mwa mashindano mengine.
imetayarishwa na Denis zadock
Kommentare