top of page
Writer's pictureOrina Ontiri

TAARIFA LEO 06/09/2015

1] Hafla ya kukusanya maoni kutoka kwa wakaazi wa Kisii ambayo ilifanyika jana Jumanne katika ukumbi wa Cultural Centre ilishuhudia watu wachache sana ambao walihudhuria kongamano hilo.


Kampeni hiyo ambayo imekuwa ikiendelea kwa muda sasa kwenye kaunti mbali mbali kote nchini, iliweza kuhudhuriwa naye mwenyekiti wa pesa za maendeleo za maeneo bunge maarufu kama CDF, Elias Mbao pamoja na mbunge wa eneo bunge la Nyaribari Masaba  Elijah Moindi ambaye pia ni mwanachama wa kamati teule ya bunge inashughulikia pesa hizo za CDF ambaye pia anawakilisha kaunti mbili za eneo la Gusii; Kisii na Nyamira. Ukumbi huo ambao kwa kawaida hujaa pomoni kunapokuwa na hafla kama hizo, ulijazwa nusu, ambapo mwenyekiti Mbao alivilaumu vyombo vilivyowajibishwa kusambaza ujumbe huo kwa kutofanya kazi yao kikamilifu. Hata hivyo, wengi waliohudhuria kongamano hilo waliunga mkono kuwe na pesa hizo za maendeleo ya maneo bunge, ila wakapendekeza kubadilishwe watu na wasimamizi ambao wanadaiwa kuwa na uhusiano na wabunge wa maeneo ya uwakilishi. Hafla hiyo ya kukusanya maoni imekuwa ikikusanya maoni kutoka kwa kaunti tatu katika kila kikao, ambapo hafla ya leo iliweza kuwakutanisha wakaazi wa kaunti za Kisii, Nyamira pamoja na kaunti ya Migori.

2]Senate wa kaunti ya Nyamira amemtaka gavana wa kaunti hiyo kuhakikisha wafanyakazi wa vibarua wanalipwa pesa zao.

Senata huyo pia amewataka wafanyikazi hao kupewa kipaumbele katika kazi ambazo zimetangazwa na kaunti hiyo. Akiongea na waandishi wa habari katika mji wa Nyamira siku ya Jumatatu, Seneta Okong’o Mong’are alishangazwa na swala hilo la kaunti hiyo kutowalipa wafanyakazi hao wa vibarua. Alisema kuwa kuna pesa zilizotengwa kushughulikia malipo ya wahudumu wote wa kaunti ambao hufanya kazi katika vitengo mbali mbali katika kaunti hiyo. Mong’are alimtaka gavana wa kaunti ya hiyo, John Nyagarama kuwajibikia maswala yanayomlenga. Alimtaka gavana kushughulikia swala hilo liloripotiwa katika vyombo vya habari kuhusiana na vibarua ambao wanahudumu katika hospitali ya Nyamira level five ambao wamekuwa wakilalamikia kutolipwa hela zao kwa muda sasa. Seneta huyo amekuwa mkosoaji mkubwa wa gavana wa kaunti hiyo yake kwa siku za hivi karibuni.

3Mbunge wa Homabay Town amewataka viongozi wote kutoka eneo pana la Nyanza Kusini ikiwemo Kisii kuunga mkono pesa za maendeleo ya maeneo bunge CDF, ili zibaki katika mikono ya wabunge.

Akiongea hiyo jana Jumanne  kwenye hafla ya kukusanya maoni kutoka kwa wakaazi wa kaunti za Kisii, Migori na Nyamira ambayo ilifanyiwa kwenye ukumbi wa umma wa Cultural Centre, Kaluma alisisitiza umuhimu wa pesa hizo ambazo alisema kuwa zimesaidia pakubwa kwa kuinua maendeleo ya maeneo ya mashinani. Aliahidi kupigana hadi mwisho kuhakikisha pesa hizo zinabaki chini ya mamlaka ya wabunge, na kuona kuwa zinasimamiwa vizuri na pia kudokeza kuwa atasimamia mswada ambao utahakikisha kuwa matapeli ambao wamekuwa wakiwekwa na viongozi flani kusimamia pesa hizo wanaondolewa ili kulisafisha jina la usimamizi wa pesa hizo. Pesa za maendeleo ya maeneo bunge zimekuwa na mzozo kati ya maseneta na magavana, huku wengi wa wananchi na viongozi wakitaka sheria maalumu kuwekwa ili kutoa uangalizi na usimamizi ulio wazi wa fedha hizo ambazo licha ya kufanya maendeleo katika mashinani, zimelaumiwa kwa kutoa mwanya kwa wabunge wengi kuwa wafisadi na kuwaajiri jamaa zao kusimamia miradi inayofadhiliwa na hela hizo.

Na katika Michezo

4Katibu mkuu wa michezo ya riadha katika viwango vya shule za msingi katika eneo la ziwa kuu Ben Ochieng’, amesema kuwa na imani wataibuka na ushindi mkubwa katika mashindano ambayo yalimalizika juzi  Jumatatu katika chuo cha Kisii. Ochieng’ alikuwa akitoa hutuba yake ya kufunga mashindano hayo yaliyozikutanisha shule zaidi ya 30  za msingi kutoka kaunti za Migori, Homabay, Siaya, Kisumu, Nyamira pamoja na mwenyeji kaunti ya Kisii, ambapo hakuficha furaha yake kufuatia hali njema ya anga ambayo iliwapa nafasi mwafaka ya kufanikisha mashindano hayo bila shida. Hata hivyo, katibu huyo alionyesha wasiwasi wake kwa wapinzani kutoka maeneo ya Bonde la Ufa ambalo alisema limekuwa mpinzani mkubwa, na kuwataka washiriki wote kuendelea kujiandaa mapema ili kuboresha matokeo hayo kufikia wiki ijayo tarehe 12 kutakapofanywa mashindano ya kitaifa. Ochieng’ hakusita kuwaomba wanafunzi walioteuliwa kutumia faida ya kuwa wenyeji wa mashindano hayo kwa kuibuka na ushindi mnono. Bado mashindano hayo hayajaamuliwa ni wapi hasa yataandaliwa kati ya uga wa michezo wa Gusii na ule wa chuo Kikuu cha Kisii, lakini Ochieng’ aliweza kudokeza kwamba huenda wakatumia uga wa Gusii kufuatia gavana wa kaunti hiyo kusema kuwa Chuo cha Kisii huenda kuwe na hafla nyingine.Mashindano hayo yataanza tena hapo kesho yakijumuisha kaunti zote.

5]Mwanafunzi wa miaka 11 alishangaza watazamaji waliojumuika katika uwanja wa michezo wa Chuo Kikuu cha Kisii siku ya Jumatatu baada ya kumenyana na zaidi ya wapinzani 50 kwenye mbio za mita 10,000 na kuibuka nambari tatu.

Mwanafunzi huyo alifuzu kuingia katika kikosi kitakachowakilisha eneo la ziwa kuu kwenye michuano ya riadha ya kitaifa ambayo itafanyika wiki ijayo. Mwanafunzi huyo, Jane Ghati kutoka shule ya msingi ya Nyabikongori katika Kaunti ya Migori, alipata upinzani mkubwa kutoka kwa wanafunzi wenzake ambao walionekana kuwa na miili mikubwa na kuwa na misuli iliyotutumka lakini mtoto huyo hakushtushwa na wenzake hadi ilipofika mzunguko wa mwisho alitoka nambari ya kama kumi na tano ambapo aliwapita wanariadha waliokuwa mbele yake na kuridhika na nambari tatu. Akiongea naYard na ARG  baada ya kukamilisha shindano hilo, Ghati alionyesha furaha kubwa kwa kuteuliwa kuwakilisha eneo la Nyanza na kusema kuwa atajitahidi ili kufanya vizuri zaidi na kushinda wenzake katika kitengo hicho. Mwenyekiti wa riadha kutoka kwenye kaunti anakotokea mwanafunzi huyo John Samwa, alisikitikia ukosefu wa msaada wa kifedha kutoka kwenye kaunti yao ya Migori, hali ambayo alitaja kuwa chanzo cha kuwasafirisha wanafunzi wachache kuwakilisha kaunti hiyo katika mashindano hayo. Lakini mwenyekiti huyo hata hivyo alionyesha moyo wa kumpa motisha mwanafunzi Ghati kutimiza ndoto yake ya kuafikia mafanikio kwenye mbio hizo za mita 10,000.

Hizi ni habari zetu sikitayarishwa na Peter Onkoba na Brighton makori 10th  June 2015 ndani ya Yard fm 104.0 fm kisii na http://www.abagusiiglobalradio.com AGR FM

1 view0 comments

Recent Posts

See All

Comments


bottom of page