top of page
Writer's pictureOrina Ontiri

yanayojiri 5/27/2015

1] Kaunti ya Kisii imetoa hadi  kuwa itasaidia taasisi zote zilioko katika kaunti  ya kisii  ili kujiendeleza kutoa mafunzo kwa  kwa vijana wa kaunti hiyo.

Akiongea hiyo jana katika taasisi ya  Nyamondo ilioko katika eneo bunge la Kitutu chache kusini Gavana wa kaunti ya Kisii James ongwae alisema kuwa serikali yake  imeweka mikakati kapambe ya kusaidia taasisi zote katika kaunti hiyo ili kuinua viwango vya masomo. ‘Serikali ya Kaunti itahakikisha kuwa taasisi zote simepata  uzaidizi unaostahili  ii kuinua viwango vya masomo kwa vijana wetu ili kujiendeleza kimasomo na kupata ujuzi wa kijiekimu kimaisha”alihoji Ongwae. Aidha, Gavana ongwae aliongezea kuwa taasisi ni chuo muhimu kwa kuwa hutoa mafunzo maalumu kwa watu na kuwawezesha  kuwa na ujuzi wa kujiendeleza kimaisha na kuwaomba watu kujiunga katika taasisi mbalimbali ili kupata  mafunzo hayo. “Vijana wengi haswa wale wamejiunga na taasisi hizo wamefaidhika pakubwa na wamejiendeleza kimaisha  kwa hivyo  vijana wote wanastahili  kujifunza jinsi ya kufanya kazi haswa za mikono ili kujiendeleza kimaisha”aliongezea Ongwae Gavana alikua  na mbunge wa eneo hilo  Momaima onyoka  ambao walitoa usaidizi wa shillingi million 3 ili taasisi hiyo iweze kujiendeleza kwa miradi mbalimbali. Kwingineko viongozi hao walihapa kushirikiana na kufanya kazi kwa pamoja ili kuinua viwango vya maendeleo  na uchumi katika kaunti ya Kisii.

2] Wanabodaboda kutoka kaunti ya Nyamira wamelalamikia uongozi wa kaunti hiyo kwa kuwa barabara nyingi  ni mbovu na hazipitiki.

Wakiongea hiyo jana wakati walikuwa wakiandamana wanabobaboda hao katika barabara ya Nyaikuro-Tombe eneo bunge la Kitutu Masaba, waliwalaumu baadhi ya viongozi kwa kutozingatia ujenzi  wa barabara katika eneo hilo. Wanabodaboda hao walisema kuwa waliamua kuandamana ili kilio chao kitasikizwe. Wakiongozwa na mwenyekiti wao  Thomas Arunda  ambaye alisema kuwa waliamua kuenda katika maandamano ili kilio chao kisikizwe kwa kuwa wao kama wanabodaboda wamesumbuka sana hasa wakati huo wa mvua nyingi inayoendelea kunyesha. Kwa sasa wamemwomba mbunge wa Kitutu Masaba kushughulikia jambo ilo kwa haraka ili kutatua shida hizo kwa haraka. Kwa kweli barabara hii haipitiki nazi hufanya kazi ngumu na pikipiki zetu kila siku hualipika kwa sababu ya barabara hii mbovu kwa hivyo tunamuomba mbunge wetu kutushughlikia jambo hilo kwa haraka “Alihoji James  Mokaya mwanabodaboda Kulingana na wanabodaboda hao ambao walikuwa na ghadhabu kubwa walioamua kulima na kupanda ndizi katika barabara hiyo  kwa kuwa  ni kama Shamba . Aidha, wameomba serikali ya kaunti ya Nyamira kushilikiana na serikali kuu  na kukarabati baadhi ya barabara ili kulahizisha uchukuzi katika kaunti hiyo. Kwingineko walisema kuwa wamama huwa na shida ya kufika hospitalini kwa sababu ya barabara mbovu na biashara imerudi chini. “wamama haswa wajawazito uogopa kupanda pikipiki zetu kwa sababu ya hali  ya barabara hizi,tunaomba serikali itukumbuke na kukarabati barabara “alihoji Momanyi Joshua.

3] Chifu wa lokesheni ya Mochenwa wadi ya Gesima eneo bunge la Kitutu Masaba amehapa kuwa wagema wanaotengeneza pombe haramu watachukuliwa hatua kali ya kisheria .

Akiongea hiyo jana ofisini mwake alisema kuwa yeye na manaibu wake watahakikisha kuwa pombe hiyo haramu imeisha katika lokesheni yake.

Kulingana na chifu magara makori pombe hiyo ndio janzo ja  familia nyingi kutengana na  vijana wengi kutoenda shule  kwa kutumia pombe hiyo, kwa sasa amewaomba wagema hao kufanya biashara nyingine kabla msumeno wa sheria kuwafikia.

4] Wakati jukwaa la dunia kuhusu jamii na mawasiliano ulimwenguni, WSIS, likiendelea huko Geneva, Uswisi imebainika kuwa idadi kubwa ya watumiaji wa mtandao wa intaneti ikiwemo mitandao ya kijamii, mathalani barani Afrika, hawana ufahamu na uelewa wa kutosha kuhusu matumizi yake na hivyo kuhatarisha usalama sio wao tu bali wa mali zao na jamaa zao. Hiyo ni kwa mujibu wa Meneja mawasiliano wa mamlaka ya mawasiliano Tanzania, TCRA Innocent Mungy ambaye anashiriki mkutano huo akiwakilisha Tanzania ambapo amesema ukosefu wa uelewa wa kutosha husababisha watu kuchapisha taarifa ambazo huangukia mikononi mwa wahalifu wa mitandaoni.

Global Radio Network

0 views0 comments

Recent Posts

See All

Comments


bottom of page